Kazi yako unayoifanya kwa wengine, labda wewe ni fundi nyumba, au fundi cherehani, au fundi umeme, au fundi telisi, na ufundi mwingine mwingi ambao sijautaja hapa.

Unafikiri huduma unayotoa kwa wateja wako ni ya uhakika? Unafikiri huyo mteja wako akikutana na fundi mwingine akafanyiwa kazi uliyomfanyia wewe, atakukumbuka na kukuona wewe bado fundi bora kwake?

Maana ipo siku utakakosekana kwa muda na huyo mteja wako atakuwa anataka huduma kwa muda huo. Atakapoenda kupata huduma sehemu nyingine atakapotoka hapo bado ataiona huduma yako ni bora zaidi?

Au atakapotoka hapo atakuwa ameona kiwango chako ni cha chini sana, na kumwona huyo aliyempa huduma ana kiwango cha juu zaidi yako. Na akafika mahali akaona kwanini alichelewa kumfahamu huyo mtu.

Hebu fikiri tu, kama unaona kabisa huyu mteja akienda mahali pengine hatakaa arudi kutokana na huduma yako mbovu unayompa. Ninakushauri sasa jirekebishe upesi, anza kufanya kazi zako kwa viwango vya juu.

Nimetoa mfano wa fundi lakini zipo huduma nyingi sana ambazo tunatoa kwa watu au jamii, tunapaswa kujitafakari sisi wenyewe. Hao watu tunaowapa huduma wakienda mahali pengine wakahudumiwa watatukumbuka na kuona hakuna zaidi yako?

Hii iwe ni changamoto yetu ya kufanya kazi zetu, au biashara zetu kwa ufanisi mkubwa, na kujua kuna watu wanafanya kama sisi. Na wanamtegemea mteja yule yule aende na kwao siku moja.

Watumishi wa Mungu hii iwe ni fikiri yetu pia, tufikiri juu ya mafundisho yetu ya neno la Mungu yana viwango vya kumfanya mshirika aone mahali alipoenda sio mahali sahihi. Na alipotoka ni mahali sahihi na Mungu yupo mahali pale/hapo.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081