
Naamini kila mmoja wetu anapenda awe na sifa fulani njema katika maisha yake, na kama kuna mtu hapendi sifa njema basi atakuwa anahitaji msaada wa kiroho.
Lakini wengi wetu tunapenda tuwe na sifa fulani njema, na sifa hizo sio za kuigiza, sifa ambazo zinaendana na yale maisha yetu tunaishi. Sifa zinazotoka ndani yetu, ambazo hufanyi kwa kulazimishwa na mtu.
Sifa njema kwa mtu haiji tu, au haioti kama uyoga, ipo gharama ambayo huyo mtu anapaswa kuitoa katika maisha yake. Yapo maeneo anapaswa kuyakataa na kumruhusu Yesu Kristo katika maisha yake.
Na Yesu Kristo akishakuwa sehemu ya maisha yake, na akajua kipi mkristo hapaswi kukifanya ili uwepo wa Mungu usiondoke kwake. Tabia njema itaanza kuwa sehemu ya huyo mtu.
Sasa ipo changamoto pia kwa mtu ambaye tayari ameshampa Yesu maisha yake, lakini bado kuna tabia fulani njema anaitamani iwe sehemu ya maisha yake ila haipati au haiji.
Unachopaswa kujua yapo mambo hayawezekani hivi hivi hadi kwa kufunga na kuomba, zipo tabia mbaya haziwezi kukuachia hadi uzichukie na uamue kuziacha kabisa.
Unachopaswa kufanya leo ni kwamba fikiri vizuri ni sifa zipi unatamani kuwa nazo, anza kuchukua hatua ndogo kabisa. Anza kuishi vile unatamani uwe.
Najua haitakuwa rahisi kwa sababu unaanza ila nakuambia anza bila kujali chochote, najua utakosea, utavunjwa moyo na watu, najua utakatishwa tamaa na ndugu, marafiki, wazazi nk. Usiogope wala usirudi nyuma, songa mbele.
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana, kwake yote yanawezekana, chukua hatua kuanza kuishi kwenye eneo unatamani uwe. Tena hahitaji kujipanga sana ni kuanza sasa, bora ukakosea utajirekebisha kuliko kuogopa kukosea huku ukiendelea kukaa mahali hupataki.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest
www.chapeotz.com
+255 759 80 80 81