
Sio jambo la kuficha, wala sio jambo la kuonea aibu kusema hadharani, ipo wazi kabisa kuwa wengi wetu ni wavivu/wazembe wa kusoma makala ndefu iliyoandikwa.
Hiyo ni makala, ukimpeleka mtu kwenye usomaji wa vitabu huko ndio unampoteza kabisa. Ataona kama umempeleka sehemu ambayo ni mateso makubwa kwake.
Hilo utakubaliana nami hasa sisi Watanzania, japo sio wote wenye tabia ya uvivu wa kusoma vitabu. Lakini asilimia kubwa ni wavivu sana na mtu yupo tayari kununua nguo kila wiki ila hawezi kukumbuka kununua kitabu kimoja kila mwezi akasoma.
Tumeshafahamu watu wengi ni wavivu kusoma, iwe makala, au iwe kitabu kizima, uvivu wa kusoma kwa wengi wetu ni mkubwa sana.
Lakini unaweza kuta mtu anachati kutwa nzima, hilo hawezi kuona tabu ila mpe kitabu atulie asome anaweza akakuona wewe ni adui yake mkubwa.
Pamoja na idadi kubwa kuwa na uvivu wa kusoma vitabu au makala au jumbe ndefu au masomo marefu. Naomba leo nikufikirishe kitu hichi hasa wewe unayesambaza ujumbe wako wa maandishi kwa watu.
Umewahi kukaa chini na kufikiri ujumbe unaoandika na kuusambaza kwa watu, huo ujumbe ukikutana na mvivu mmoja ambaye huwa hapendi kusoma maneno mengi.
Atakapokutana na ujumbe wako na akajishawishi kusoma, unaweza ukamfanya akasimamisha shughuli zake na kukaa chini kusoma kile umeandika? Hii iwe ni fikiri yako ya leo.
Huwa hawasomi jumbe zako sawa, unafikiri siku wakisoma watavutiwa kuendelea kusoma? Na kama watavutiwa kusoma unafikiri watatamani kuendelea kusoma zaidi?
Kwanini nakufikirikisha haya, napenda ukiwa unaandika masomo yako au makala zako utulie na utumie akili zako zote alizokupa Mungu. Hupaswi kuandika kwa kulipua, unapaswa kuandika ujumbe wako ukiwa na picha kubwa ndani yako.
Picha ambayo inamtazama mvivu mmoja aliyekaa mahali alafu anahitaji msaada wa kutoka hapo alipo na kwenda sehemu nyingine.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081