Unafikiri unavyoumia ni kwa sababu ya kuonewa au ni kwa sababu ya uelewa wako wa mambo ulivyo. Kauli hii inaweza isiwe njema sana kwako ila ndio ukweli wenyewe ulivyo.

Inawezekana kabisa hilo unaloona umeonewa sio kweli umeonewa isipokuwa ni vile uelewa wako ulivyo.

Ama inawezekana kabisa kwa kutojua kwako neno la Mungu linasemaje kuhusu hilo, au kwa kutokujua nyakati, ukaona unaonewa kumbe sio kuonewa imeruhusiwa iwe hivyo.

Vipo vitu ambavyo huwezi kukwepa katika maisha yako, maana vimeratibiwa na Mungu mwenyewe vikupate/vikutokee. Ili jina lake litukuzwe au liinuliwe kupitia hayo unayopitia au uliyofanyiwa na watu.

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, yapo mambo yanatutokea sio kwa sababu ya uonevu wa watu, au sio kwa sababu ya wivu wa watu.

Yanatutokea kwa sababu ilipaswa iwe hivyo, ama yanatutokea kwa sababu ya kukosa kwetu maarifa sahihi, au kwa kiburi chetu tulichonacho, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yetu.

Hebu jiulize hapo ulipo, hicho ulichokuwa unaona unaonewa kabla hujasoma huu ujumbe na hadi sasa una huzuni moyoni mwako, au una hasira kifuani mwako. Unafikiri umeonewa au ni sahihi kutokana na moyo wako unavyokushuhudia.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest
www.chapeotz.com
+255 759 80 80 81