Yesu asifiwe, ninamshukuru Mungu kwa uzima alionipa siku ya leo, na kunipa nafasi ya kukuletea ujumbe huu.

Tumekuwa watu wa kusikia maneno mazuri yakisemwa juu ya mtu fulani, bila kuzipima hizo sifa anazopewa mtu ni za kweli. Ama ametengeneza watu wa kumsemea vizuri lakini sivyo alivyo huyo mtu.

Tumekuwa watu wa kusikia maneno mabaya au sifa mbaya juu ya mtu fulani, bila kukaa chini na kufikiri kinachosemwa juu ya huyo mtu ni cha kweli ama anachafuliwa tu. Ili aonekane hafai kwa maslahi ya mtu binafsi.

Hebu fikiri mangapi umewahi kusikia juu ya mtu fulani, alafu baadaye ukaja kugundua haikuwa kweli. Na wewe tayari ulishatia maneno yako kwa huyo mtu.

Hebu fikiri mambo uliyowahi kuyasikia na yakakutia hofu kubwa sana katika maisha yako, lakini baadaye  hayajakupata kama ulivyokuwa unawaza yatakupata.

Ukishafikiri hayo sasa anza kuwa mtu wa tofauti kabisa, mtu ambaye habebi habari alizozisikia juu juu na kuanza kuzisambaza ovyo.

Na kuwa mtu mkomavu usiyepelekeshwa na habari za kusikia bila kuwa na uhakika nazo ukaanza kupaniki na kukupa hofu kubwa.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com
+255759808081