
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo, siku nyingine tena Bwana ametupa nafasi ya kuifikia. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa nafasi hii.
Vipo vitu katika maisha yetu ya kila siku huwa tunaambiwa, vinaweza kuwa ni vitu vizuri, na vinaweza kuwa vitu vibaya kwetu.
Ikiwa ni taarifa nzuri kwako, je huwa una kitu ambacho kinakupa uhakika kuhusu hiyo taarifa?
Kufikiri ni muhimu sana, maana zipo taarifa zilionekana njema kwenye masikio ya watu. Baadaye zilikuja kugeuka msiba mkubwa kwao.
Unachoambiwa haijalishi ni kizuri sana kwako, kama huna maarifa juu ya hicho unachoambiwa. Bado hicho unachoambiwa hakiwezi kuwa kitu chema kwako.
Hata zile taarifa tunazoona ni mbaya kwetu, kama hatuna uelewa nazo hatupaswi kuzichukulia kwa upande wa ubaya tu. Maana kuna mengine yanaonekana ni mabaya kutokana na ufahamu wetu ila kwenye uhalisia sio mabaya.
Fikiri vizuri kuhusu ulichoambiwa, usikichukulie kwa namna ya hasi, wala usifikiri kwa namna ya chanya. Tulia kufikiri, kama unahitaji kuliombea fanya hivyo, kama unahitaji kupata ushauri kwa unaowaamini fanya hivyo.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081