Yesu asifiwe, Mungu ni mwema ametupa nafasi nyingine ya kuiona siku ya leo, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu.

Kusema kwa maneno utafanya inaweza isiwe kazi ngumu sana kwa anayesema, lakini ukija kwenye kutenda anaweza asitende kama alivyotamka.

Yapo mambo mengine yanawatia watu hofu pasipo kujaribu, anaweza akawa alijaribu mwingine. Huyo akawa anamtia hofu ya kutojaribu na yeye.

Ama amewahi kujaribu kufanya mara moja akashindwa, hiyo imekuwa nukuu yake ya kushindwa kujaribu tena.

Hebu nikufikirishe leo, je umewahi kujaribu kufanya hicho kinachokutia hofu? Je umewahi kujaribu kufanya hicho unachokiweka kwenye malengo yako ya kila mwaka?

Katika kufikiri kwako usivunjwe moyo na ile sauti inayokuambia ukijaribu kufanya tu lazima ushindwe, hiyo isikutishe cha kufanya ni kujaribu kufanya.

Hebu jaribu kufanya jambo unalolitamani katika maisha yako, bila kujalisha hali uliyonayo sasa. Bila kusubiri maandalizi makubwa sana, wewe amua kufanya.

Unatamani kuombea mgonjwa apone na hujawahi kufanya hivyo, anza leo kuombea wagonjwa kwa ujasiri. Fahamu anayeponya sio wewe, bali ni Yesu Kristo ndiye anayeponya.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com