
Yesu asifiwe, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyotupa siku ya leo.
Yapo mambo ambayo yanamfanya mtu alalamike, labda kwa kutendewa au kufanyiwa ndivyo sivyo, hii inamfanya mtu alalamike.
Wapo wengine kazi yao ni kulalamika tu, hata kama wanayoyalalamikia walipaswa kuchukua hatua wenyewe. Utakuta wanawalalamikia wengine.
Uwe unalalamika kwa kutendewa vibaya, ama uwe unalalamika kwa jambo ulipaswa kuhusika mwenyewe ila unawatupia wengine lawama.
Unapaswa kufikiri, kulalamika kwako kunaweza kuzalisha matokeo gani? Kulalamika kwako kunaweza kukusaidia kwenye shida iliyokupata?
Kama ndio endelea kulalamika bila kuchukua hatua yeyote, na kama ni hapana acha Mara moja kulalamika na chukua hatua.
Vipo vitu hata ulalamike usiku na mchana hakuna kitu utabadilisha zaidi utaonekana kwa namna ambayo inaweza kukushusha viwango vyako au heshima yako.
Kwanini ufikiri kuhusu hili, hii itakusaidia kuwa na kiasi, hii itakusaidia kuacha kulalamika kwa kitu ambacho unaweza ukakiondoa/ukakirekebisha mwenyewe.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
Blog: www.chapeotz.com
WhatsApp: +255759808081