Shalom Mtumishii! Namshukuru Mungu kwa ajili ya kundi la Chapeo Ya Wokovu. Mungu amekuwa mwema kwangu, nimeziona nguvu na uweza wake  kwa imani yangu ndogo sana kulinganisha na Neno ambalo umekuwa ukilituma kila siku.

Mwaka jana nilipata shida ya mguu wa kushoto baada ya kuanguka kwenye ngazi nikiwa ofisini, shouk niliyokuwa nayo sikuita mama niliita Yesu! Nilienda Hospital ya Mwananchi &Bugando bila nafuu na nilizidi kuumwa sana mguu.

Nilikuwa nafuatilia sana somo la kila siku la SOMA NENO UKUE KIROHO (https://bit.ly/2UA8i2p) na maombi pamoja na tafakari ya kila siku ya Neno la Mungu, niliendelea kutumia dawa lakini sikupona, niliingia maombi yakufunga kwa wiki nzima.

Kisha nikaamua kwenda Agha khan kwa check zaidi, nilichukua vipimo na mguu ulionekana mfupaa wa goti ulisogea, hivyo nilipewa Bed Rest ya mwezi mzima kupumzisha mguu.

Niliumia kwa kuwa sikuweza kufanya huduma wala chochote zaidi ya kulala kwa ajili ya mguu, lakini nilijua ni kazi ya adui anapambana kuondoa utayari wangu hivyo niliendelea kutumia dawa na mapumziko.

Nilisoma Somo la 305 (https://bit.ly/2kyyYDt) ambapo lilinitia nguvu na kwa kuwa zilibaki siku mbili kufungua ile stabilizer au kumaliza mapumziko. Nilirudi Hospital nikaanza mazoezi hapo hapo Agha khan, kadri nilivyokuwa ninafanya zoezi maumivu yalizidi nikashindwa kutembea hata kukanyaga chini.

Hivyo nikaambiwa natakiwa niende KCMC niliumia sana na nikamshirikisha mama mchungaji Maganga ambaye yupo group la whatsApp la Chapeo Ya Wokovu. Kwa kuwa ananifahamu, tunafahamiana ni mlezi wangu wa kiroho.

Pia alitamani niombe maombi ya safari kutoka Mwanza kwenda Moshi ila ndani yangu nikawa sijisikii kufanya hivyo, nilimwambia tu asiwashirikishe  wana group. Nilisafiri nikaenda Moshi, nikawasili KCMC na nilipofika nilikuwa nasoma somo la 405 (https://bit.ly/2Gt9stL)

Nilimwomba Mungu anisaidie nipone kwani nilikuwa naumwa sikanyagi chini, nilifika nikawa na barua ya kipimo cha MRI wakaniambia kimeharibika natakiwa niende Arusha, na Arusha kipimo nilifanyia hospital inaitwa Nsk.

Majibu yalionyesha wakati naruka mishipa ilikatika na ndiyo inasababisha maumivu na njia yakufanya ni operations tu, hivyo nikaambiwa natakiwa kufanyiwa operation. Nikarudisha majibu KCMC kusubiri operation day.

Nilipata somo ambalo lilikuwa likizungumzia Mafarisayo walivyokuwa wanamdhihaki Mungu, niliendelea kusoma yale maneno kiukweli hata ile kutafakari nilidrop ukiangalia utaona. Niliandikiwa siku yakufanyiwa nilijaza fomu ila nikamwambia Mungu kama uishivyo mimi sitakubali operation, hii utafanyiwa wewe siyo mimi.

Niliriport nikawa nasubir kufanyiwa operation, nikakaa wakati nataka kuingia chumba cha operation nilisoma somo la hiyo siku, yaani SOMA NENO UKUE KIROHO na ndani yangu ikaumbika imani zaidi. Nilisoma nikabadilisha nguo nikazima simu nikaingia ndani, kiukweli pumzi na moyoni sikuogopa japo sijui hata operation ingekuwaje.

Nilikaa Doctor aliingia akasema asee kuna sindano nadhani itakusaidia, nilichomwa sindano na nikawa Bedrest kwa siku NNE na drip, sikuwa naweza kuamka maana nilikuwa na drip na sindano. Niliambiwa wangeniangalia kwa siku NNE kweli niliendelea kufuatilia Neno la kila siku wakati mwingine walinisomea.

Maana nilikuwa nalala na Doctor alikuwa anashauri nisitumie simu nipumzike, baada ya siku NNE niliruhusiwa, nikaanza kutembea kufanya zoezi. Afya iliendelea kuimarika siku hadi siku, hadi nikawa mzima, yaani nimepona.

Na sasa nimerudi kazini, imebakia nafanya mazoezi madogo madogo, namwadhimisha Mungu kwa ajili ya hili. Wapendwa tusione kwamba jumbe zinazorushwa ni ndefu ukatapa uvivu kusoma, mimi nimepona kupitia Neno la kila siku, sifa na utukufu nampa Kristo.

Mungu akubariki sana.
Imeandikwa na
Furaha Mghase.
www.chapeotz.com