“Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili”, Zek 6:13 SUV.

Bwana alimwamuru Zekaria kutengeneza taji ya fedha na dhahabu na kuiweka katika kichwa cha Yoshua kuhani mkuu.

Kuvikwa taji kwa Yoshua kunaashiria kwenye kuvikwa taji na kutawala kwa Yesu, ambaye ni “Chipukizi” ambaye ni masihi.

“Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda”, Isa 11:1 SUV.

Yesu angekuwa kuhani na mfalme; kwanza angefanya kazi yake ya kikuhani, alafu angetawala.

“Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake”, Isa 53:10 SUV.

Kwa wakati huu, Yesu ni amani yetu na katika yeye tunapata ufalme wa Mungu ambao uko katika haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

“Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu”, Rum 14:17 SUV.

Kutimizwa kikamilifu kwa utawala wa Kristo kunaanza katika ile miaka elfu moja, atakapotawala duniani utawala wa amani.

Mungu akubariki sana
Soma neno ukue kiroho
Samson Ernest
+255759808081