Ukifuatilia hili la kuonekana mtu fulani na wengine hawapaswi kuonekana hata kama wamefanya.

Utaona asili hii ya kiMungu ipo kwa watu wake, baadhi ya watu wapo tayari kukuondoa kwenye nafasi yako, kwa sababu ya kutaka kuonekana wewe badala ya wao.

Wapo viongozi wa ngazi za juu wanapenda kuonekana wao wamefanya, hata kama ukweli unajulikana kuwa watu wake wa chini ndio waliofanya hilo.

Sasa yeye kama kiongozi mkubwa anapenda kuona yeye ndiye amefanya hiyo shughuli.

Kwa upande mwingine inapaswa kuwa hivyo kabisa, na ukishaelewa hili utakaa na kiongozi wako wa juu vizuri sana bila shida yeyote.

Hili tunaliona kwa Mungu mwenyewe anampa maagizo Gideon awachunje wanajeshi wake.

Lengo haswa la kufanya hivyo ni nini? Mungu alitaka wasije wakajisifu wao na kuona wingi wao ndio uliofanya washinde vita.

Wangeona hivyo wasingeweza kutambua nafasi ya Mungu katika ushindi waliopata kwenye vita.

Rejea: BWANA akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. AMU. 7:2 SUV.

Unaona hapo, Mungu siku zote huwa anapenda yeye ndiye aonekane amefanya. Maana yeye ndiye Mungu wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Sio hilo tu, Mungu hutaka matendo yake makuu aliyoyafanya kwa mwanadamu. Sifa na utukufu zimrudie yeye Yesu Kristo.

Hili liwe somo kwetu, litatusaidia sana katika maisha yetu ya kiroho na kimwili.

Mungu akubariki sana.
Samson Ernest.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana.