“Ibrahimu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi”, Mwa 23:7 SUV.
Inaonyesha kwamba sehemu pekee aliyopewa Ibrahimu na kuimiliki kuwa Mali yake huko Kanaani, lilikuwa kaburi na eneo alilomzikia mke wake Sarah.
“Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu”, Ebr 11:9-10 SUV.
Uzao wake hukupata nafasi ya kuimiliki nchi ya ahadi Hadi kipindi cha Yoshua, kipindi cha Yoshua ndio ilikuwa halali yao rasmi kumiliki.
Baada ya kuona historia hiyo kwa ufupi, kuna jambo la msingi sana hapa napenda ujifunze na likusaidie kwenye maisha yako.
Pamoja na Ibrahimu kutambuliwa kuwa mtu mkuu na anayeheshimika sana, hakuacha unyenyekevu wake.
“Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako”, Mwa 23:6 SUV.
Baada ya maneno haya tumwona Ibrahimu alionyesha ishara ya unyenyekevu baada ya kupewa sehemu ya kuzika mke wake na ndugu zake, mtu ambaye alikuwa anaheshimika hakutumia nafasi yake kuacha mambo ya msingi.
Kuinama mbele za watu au kusujudi mbele za watu ni ishara ya unyenyekevu, kuwashukuru watu na kutambua mchango wao ni ishara njema mbele za watu na Mungu.
Nafasi zetu tusipokuwa nazo makini zinaweza kuondoa unyenyekevu wetu kwa watu, watu wanaweza kututendea mema tukaacha kushuka na kuonyesha shukrani kwao.
Nyenyekea, washukuru watu, usione hiyo kazi ni ya watu wa chini, watu wasio na cheo chochote, utakuwa umekosea kuwaza au kufikiri. Kuonyesha unyenyekevu mbele za watu inawaachia alama njema kwenye mioyo yao.
Usionyeshe kupuuza jambo jema ulilosaidiwa au kufanyiwa na ndugu wengine, washukuru na kuonyesha unyenyekevu mbele yao kutokana na utamaduni wenu bila kujalisha wana nafasi fulani katika jamii au hawana.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081