Ninamshukuru Mungu Kwa Mambo Makuu Ambayo Amenitendea.
Nina ushuhuda mfupi ambao naamini utaenda kumwinua mtu mmoja kati yetu.
Ni ukweli kwamba sikuwa na huduma ambayo nilikuwa naona kuwa hii ndiyo huduma niliyoitiwa kuifanya hapa duniani nilikuwa sielewi kabisa.
Ilikuwa mwaka 2016, nilipojiunga na kundi la wasap la chapeo ya wokovu la kusoma neno la Mungu kila siku. Nikaanza kujibidiisha kusoma Neno la Mungu, sikujua kwamba ndio ulikuwa wakati wangu wa kuandaliwa.
Niliendelea kuweka bidii lakini siku moja tulipokuwa tunasoma kitabu cha *Ezra 3* siku hiyo siwezi kuisahau kwenye maisha yangu yote, Mungu alinisemesha kwa namna ambayo iliniuma sana ndani yangu na kumbe huo ndio ulikuwa mwanzo wa huduma ambayo Mungu alikuwa anaiandaa ndani yangu.
Niliendelea kuweka bidii sana sana kwenye Neno la Mungu, na kufocus zaidi kwenye kile ambacho Mungu amenisemesha.
Zaidi sana hata sasa Mungu amenisaidia kufikia lengo la huduma hii aliyoniita nayo sasa ninamtumikia Mungu kanisa la FPCT singida Mjini Kati (STCC)
Nimekuwekea kaclip kadogo hapa chini, unaweza kutazama ukashuhudia jinsi Mungu alivyoniinua kutoka huku Chapeo Ya Wokovu.
Unaweza kunisapoti kwa ku subscribe na kushare watu wengine pia wajionee pia.
Bonyeza link hii ==>>https://youtu.be/-79p7L7EGJ4
Na Mungu akubariki sana unaweza ukatembelea ukurasa wa Facebook page ya Singida town center church ukajionea matukio mengine mazuri na Mungu akubariki sana.
Samwel Justine
+255 762 303 577