Unaweza kufikiri jambo fulani haliwezekani kabisa kutokana na historia yake ilivyo.

Macho yetu yanaweza kutudanganya kuwa mambo fulani hayawezekani kabisa.

Tunaweza kuwaendea watu wengine kuomba watusaidie jambo fulani gumu, likaonekana kama jambo zito kwao.

Lakini napenda kukuambia kwamba hilo jambo sio kana kwamba haliwezekani. Isipokuwa watu wanataka kujua nini watapata baada ya kufanikisha hilo unalotaka/unalopenda lifanyike.

Hili tunajifunza kwa Kalebu alitangaza wazi atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa atampa binti yake awe mke wake.

Rejea: Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe. YOS. 15:16 SUV.

Kweli baada ya kutangaza zawadi nono ya mke, tunaona Kiriath-seferi ilipigwe.

Rejea: Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe. YOS. 15:17 SUV.

Hii inatufundisha jambo kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku, yapo mambo bila kutangaza dau hayawezi kufanikiwa.

Hasa kama unafanya kazi na timu yako, ili waweze kupeleka kampuni mbele watangazie dau nono.

Iwe kweli na uitoe hiyo zawadi uliyowaahidia watu, epuka uongo, kile umeahidi hakikisha unakitoa.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com