Tunapojikuta tupo katikati ya changamoto nzito/Ngamu, tusiwe wepesi wa kukata tamaa, tena mbaya zaidi kama utakata tamaa na kuachana na kujishughulisha na mambo ya Mungu. Itakuwa ni hatari kubwa sana kwako, maana utaenda kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa na wakati muujiza wako ulikuwa upo mikononi mwako.

Hatutazuia mambo mabaya yasitupate, hatuwezi kabisa kusema tukiokoka hatuwezi kupatwa na mambo magumu ya kuvunja moyo. Tena uliokoka ndio unakuwa unapitishwa kwenye madarasa mbalimbali ya kujaribiwa.

Kinachojaribiwa ni imani yako, mambo yote yanayokutekea yanapima kile unasema kinaendana na uhalisia wenyewe. Maana kuna watu wanasema wameokoka ila ukweli kabisa hawana imani ndani yao, hawaamini kama Yesu Kristo anaweza kuwasaidia.

Siwezi kujua hapo ulipo unapitishwa kwenye ngumu gani, mambo ni mengi sana ambayo mtu anaweza jikuta anapitishwa wakati huo. Lakini pamoja na kupitishwa kwenye magumu mbalimbali, tunapaswa kujua yu Mungu upande wetu.

Haijalishi hapo ulipo unapita kwenye hali gani ya kutisha sana, amini Mungu yupo pamoja na wewe. Najua moyoni unaweza kukataa hili, hasa kama hilo jambo limechukua muda mrefu. Kutokuamini kwako hakuwezi kubadilisha ukweli huu.

Rejea: Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. ISA. 43:2 SUV.

Mateso uliyonayo sasa, Bwana atakuoa nayo, wakati unaopitia haijalishi Mungu atakuvusha salama. Kitu cha muhimu kwako ni kuendelea kumwamini Yesu Kristo, fanya yote ila usiache ibada.

Ukiwa na Neno la Mungu la kutosha moyoni mwako la kutosha, lazima maneno kama haya yatakusaidia kuvuka kwenye wakati mgumu unaopitia sasa hivi. Ukikosa Neno la Mungu ni kukosa nyezo muhimu sana katika maisha yako.

Ikiwa utapitishwa kwenye moto mkali au ukiwa unapitishwa sasa kwenye magumu, usiogope, unaye Mungu wa kweli anayeweza kukusaidia kuvuka maeneo mbalimbali.

Mungu akubariki sana.

Chapeo Ya Wokovu

www.chapeotz.com

+25579808081