Amri kali inaweza kutolewa na mkuu fulani kutokana na nafasi yake, watu wakaitekeleza kwa haraka sana kutokana na msisitizo au maagizo waliyopewa. Uwezakano mpango huo ukafanikiwa kabisa kufanyika kwa walengwa.

Lakini  pamoja na amri kali, yupo mtu anaweza kuhakikisha hafuati kama anavyoamriwa kutokana na thamani ya kile alichonacho wakati huo. Haijalishi watu watakuwa wametoa sana vitu vyao, kama mhusika anaona akilitoa hilo atakuwa ameokesea sana wala hatafungwa na kitu.

Wakati mwingine tunaweza kufanya mambo kwa rafu sana kutokana na kutokujua thamani ya kile tulichonacho kina uzuri gani, mtu akishajua kitu alichonacho ni cha thamani sana. Hata kama tabia ya hicho kitu huwa kinaharibika haraka kikiwekwa vibaya, kama kina thamani kubwa kitatuzwa sana.

Pamoja na agizo la mfalme kuua watoto wote wa kiume, mama yake na Musa wakati ndio Musa mwenyewe ndio amezaliwa siku sio nyingi. Mama yake aliona mtoto wake ni mzuri sana, akaona hawezi kumtoa auawe huko nje.

Alichofanya ni kumficha yule mtoto kwa miezi mitatu, mama yake alikuwa anamwona mzuri na Mungu alikuwa na kusudi lake na Musa. Bila kujalisha watoto wangapi wameuawa, idadi ilikuwa kubwa ila halikumtisha amtoe mtoto wake.

Rejea: Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. EBR. 11:23 SUV.

Hii inatufundisha mengi sana tukiwa kama wakristo wenye safari ya kwenda mbinguni, jambo lolote likiwa zuri kwako unaweza kulilinda kwa gharama yeyote ile. Haitajalisha kuna matisho gani yametokea au yatatokea, wewe utaendelea kusimama.

Wakati mwingine tunaleta sababu nyingi kutokana na kutojali kile ambacho tunakihitaji au ambacho tunacho tayari, lakini hakina faida yeyote. Lakini mtu akishajua umhimu wa jambo lolote lile hawezi kukwamishwa na vitisho vyovyote vile.

Uwe na uhakika kitu chochote utakachokiona cha maana sana au kizuri sana kwako, ujue hicho kitu huwezi kukitoa kienyeji kwa sababu haupo tayari kupoteza muda.

Unaweza kuliweka suala la kusoma Neno la Mungu kama utakuwa umejiwekea nidhamu na kulipenda, utaona haupo tayari kulipoteza bali utakuwa upande wa kufanya maamzi magumu.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com