
Zipo nyakati tunaweza kupitia kwenye maisha yetu, nyakati kama hizi tunakuwa na maswali mengi wakati mwingine huwa tunajikuta tunaanza kufikiri labda tulikosea kumwamini Yesu Kristo.
Tunaanza kufikiri hivyo kutokana na mambo mbalimbali mabaya yanayotupata katika maisha yetu ya wokovu, tunakuwa hatuna majibu yake. Mbaya zaidi iwe kusoma Neno la Mungu hakupo kwa mtu mmoja mmoja anayepatwa na hayo.
Ndugu usishangae utapokutakana na watu wanakudhihaki juu ya imani yako, huenda hapo ulipo unaishi maisha matakatifu yenye misimamo ya kiMungu. Kuishi hivyo inaweza isiwe baraka kwa wengine, badala yake inaweza ikawa chanzo cha wewe kukosa furaha.
Kweli usipokuwa makini, ama usipokuwa na Neno la Mungu la kutosha moyoni mwako, unaweza kujikuta unakuwa mtu wa majuto katika maisha yako. Unapokuwa kwenye kipindi cha majuto, inakuwa ngumu hata kuyafurahia maisha yako ya wokovu.
Kwanini nakueleza haya? Nakueleza haya kwa sababu nyingi sana mojawapo ni kutotetereka pale mabadiliko yeyote yatakayotokea katika maisha yako ya wokovu. Pia ni kutopata mahangaiko moyoni mwako pale utakapoona watu wanakudhihaki.
Maandiko yapo wazi juu ya hili, wale watu ambao wanaishi maisha yasiyompendeza Kristo, ndio watu ambao wanakuwa wanajivunia kuhusu yale mambo mabaya wanayoyafanya. Na kuwa kero kwa wengine waliomwamini Yesu Kristo.
Rejea: Ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. YUD. 1:18 SUV.
Usitishwe na watu vile unavyoishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu, wakaja wakaanza kukudhihaki au kukukejeli juu ya imani yako. Vile unavyozidi kumtafuta Mungu kwa bidii ndivyo unavyozidi kuongeza idadi ya wanaokudhihaki.
Pamoja na hayo yote hupaswi kushangaa kabisa na kuanza kurudi nyuma, fahamu kwamba hayo mambo yapo kwa watu waliomkabidhi Yesu Kristo maisha yao.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com