Alama nzuri inaweza kumbeba au inaweza kumsaidia mtu wakati ambao hakutarajia kama ungeweza kukutana na jambo kama hilo. Ni ule wakati ambao ulikuwa unawekeza kufanya mambo mazuri kwa wengine au mbele za Mungu, bila kujalisha wakati huo hakukuwa anaelewa sana.

Alama inamfanya mtu apokelewe vizuri mahali ambapo asingekuwa kupokelewa kwa namna ambayo ingekuwa ngumu sana kwake. Lakini alama ina uwezo wa kusema yenyewe pasipo hata wewe kusema jambo lolote.

Muhimu sana kuweka alama katika maisha yako, na muhimu sana kuweka alama katika maisha ya watu wengine, alama ambayo itawateza kukufanya uendelee kuishi siku zote.

Kuweka alama kwenye maisha yako usije ukawaza labda ni jambo kubwa sana, alama inaweza likawa jambo lolote la kawaida kabisa ila likaleta baraka kwa wengine.

Alama inaweza kumwokoa mtu na hatari mahali ambapo asingefikiri kama angesaidika na hilo jambo wakati huo, kwahiyo unaweza kuona ni jinsi gani ilivyo.

Rejea: Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. UFU. 9:4 SUV.

Alama ni jambo la kiMungu kabisa, ukisoma hili unapata kitu ambacho hata Mungu mwenyewe anajua umhimu wa kuweka alama. Maana hapa muhuri ilikuwa ni alama ya kuwasaidia wasiweze kudhuriwa.

Kuishi Vizuri na watu, huo ni muhuri wako kwao, au hiyo ni alama kwako na kwao, cha kufurahisha zaidi ni alama inayojulikana na Mungu mwenyewe. Kumbuka hii ni kanuni ya kiMungu na si ya kizembe.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com