Kama unalipwa mshahara wako, alafu wenzako wote majina yao yapo kwenye karatasi la malipo ya mshahara wako. Wewe ambaye jina lako halipo unaweza kupata shida sana kwenye moyo wako.

Utajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na hilo ila ukitulia utaona kuna shida mahali na hiyo shida inaweza kutatulika kama utaishughulikia.

Ndivyo ilivyo na mambo ya kiroho, ukikosekana kwenye kitabu cha uzima, unaweza kujikuta unajisikitikia na kulia tu.

Shida wa hili ukishakufa huwezi kurekebisha chochote ila ukiwa mzima unaweza kuweka mazingira vizuri jina lako likawepo kwenye kitabu cha uzima.

Rejea: Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako. UFU. 17:8 SUV.

Omba usikutane na hili kasheshe la kukosekana kwenye kitabu cha uzima, itakuwa ni kilio kisichokuwa na mwisho wake.

Hakikisha jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima wa milele, unachopaswa kufanya ni kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Kama umeshampokea Yesu Kristo, umebakisha kazi ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu, yaani maisha matakatifu.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo
Samson Ernest
www.chapeotz.com