Vijana wengi sana wamekuwa wakipata shida pale anapokuwa na rafiki yake wanayeelekea kwenye hatua ya uchumba.

Mara nyingi sana utakuta dada anamlazimisha kaka waoane, na kaka utamkuta anahaingaika sana na binti ili waweze kufanya mambo machache waweze kufunga ndoa.

Sasa hapa unaweza ukamkuta kaka anamlazimisha dada waoane, lakini huyo dada wala hana habari hiyo ya kuwa mke.

Unapoona unapata shida kuhusu kuoana na mwenzako, ujue upendo wenu haupo vizuri, utasema inawezekana vipi mtu niliyekaa naye kipindi cha kutosha asiwe anakupenda?

Mtu aliyependa sawa sawa, huhitaji kumsukuma, yeye mwenyewe ndio atakuwa anafanya kila jitihada kuhakikisha mambo yanakaa vizuri.

Rejea: Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu. MWA. 34:11‭-‬12 SUV.

Unaona hapo, huyu Shekemu alikuwa tayari kufanya jambo lolote atakaloambiwa na wazazi wa binti yao.

Ndivyo ilivyo na kwetu leo, mtu akipenda kweli kweli mambo mengine huwa sio jambo la kumfanya ashindwe.

Ukiona mahusiano uliyonayo hayana sifa nzuri, yaani unakesha kuyahangaikia yawe mazuri lakini mwenzeko hana habari yeyote. Ujue hapo kuna shida.

Mungu atusaidie sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest
www.chapeotz.com