Uwe Tayari Kubadilika Utakapoijua Kweli Ya Mungu.
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai, siku nyingine tena mpya kabisa Bwana wetu Yesu ametupa kibali tena kuiona tena leo. Sifa na utukufu tumrudishie yeye kwa ajili ya kuedelea kutupa uzima wake bure kabisa.
Ukianza kusoma Neno la Mungu maana yake umechagua kuijua kweli ya Mungu, na unapaswa kukubaliana na kile ambacho Mungu atakuelekeza kupitia Neno lake.
Kama umechagua kuijua kweli ila haupo tayari kubadilika kupitia kweli hiyo, huna tofauti na mtu asiyejua kweli. Ila wewe unaweza kuwa na hatari zaidi maana unajua iliyo kweli ila huitaki kuifuata.
Neno la Mungu halitakuwa na msaada kwetu kama tunalisoma huku tunaendelea kusimamia misimamo yetu ya kidini. Ambayo inatufanya mpaka tunaona Neno la Mungu halipo sawa kabisa kutokana na tulivyomezeshwa mambo fulani.
Haijalishi ulizoezwa kitu/jambo fulani ni Sahihi kwako kufanya na kuliishi, ikiwa hilo jambo lipo kinyume na Neno la Mungu lazima ukubali kubadilika.
Shida inakuja pale unapotaka kulazimisha neno la Mungu lifuate unavyotaka wewe na si linavyotaka yenyewe. Hapo ndipo utakapoanza kupoteza mwelekeo wako binafsi na utaona haina maana tena kwako kusoma Neno la Mungu.
Kila mmoja wetu Mungu anaweza kumfunulia neno lake kwa mazingira husika likamsaidia kabisa, ila maana ya kufunuliwa hilo Neno hakuwezi kuwa nje ya maana halisi ya Neno la Mungu.
Unapojikuta unapingana/kulikataa Neno la Mungu alafu unasema unamwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Fahamu umejaza sumu mbaya ndani yako, na sumu hii itaendelea kukumaliza taratibu.
Unachopaswa kufanya ni kukubali kweli ya Mungu, haijalishi hilo jambo litakuwa nje ya marajio yako. Ila kwa kuwa umeamua kujifunza mwenyewe, amua kweli kujifunza bila kusukumwa ili iwe rahisi kwako kubadilika.
Chagua kujifunza Neno la Mungu, kuwa tayari kubadilika pale unapounywa na Neno la Mungu.
Mungu akubariki sana, usiache kutembelea ukurasa wetu kwa masomo mengine mazuri.
Chapeo Ya Wokovu.
+255759808081.
chapeo@chapeotz.com