Sio ajabu kumkuta mtu akiomba kupitia wafu wamsaidie jambo.

Utakuta mtu amefiwa na babu/bibi yake siku nyingi ila  atamwomba bibi/babu yake(mfu) amsaidie.

Utakuta mtu anamwomba mtu fulani aliyefariki dunia siku nyingi. Akiwa na imani kuwa wafu/mfu anaweza kumpatia majibu ya matatizo yake.

Wapo wengine wanasema wanaomba mizimu ya  mababu zao. Wakiwa na imani watapata majibu ya mahitaji yao.

Nikueleze kwamba kufanya hivyo ni dhambi mbele za Mungu.

Mungu alishakataza tangu kipindi cha Musa, na hadi sasa agano jipya hakuna mahali anaruhusu watu waombe wafu wawasaidie.

Rejea: wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. KUM. 18:11 SUV.

Kama unaomba mfu akusaidie shida yako, ujue unakosea sana.

Mfu hawezi kukusaidia chochote, tena kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu wetu kama tunavyosoma hapa.

Rejea: Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. KUM. 18:12 SUV.

Hakuna mfu yeyote anaweza kukujibu/kukusaidia mahitaji yako, mwombe Yesu akusaidie na sio wafu.

Jina la Yesu litukuzwe.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com