
■Usifanye huduma ya Mungu kwa lengo la kupata umaarufu wa dunia hii.
■Usifanye huduma ya Mungu kwa lengo la kutafuta cheo kanisani kwako.
■Usifanye huduma ya Mungu kwa lengo la upate pesa.
Kufanya kazi ya Mungu kwa mtazamo huo niliokutajia na mingine mingi nisiyoitaja, pale utakapokosa lile ulikuwa unalitarajia utaishia kurudi nyuma, kuumia na kulaumu watu wengine kuwa hawakutendei/hawajakutendea haki.
●Elewa kwamba hatujitoi kumtumikia Mungu wetu kwa sababu ya upungufu wa fedha.
●Elewa kwamba hatujitoi kumtumikia Mungu kwa viwango kuutafuta umaarufu wa dunia hii.
●Elewa kwamba hatujitoi kumtumikia Mungu kwa kutafuta cheo.
Hayo yote ni haki yetu kuyapata, lakini sio lengo la Yesu alilotuitia kumtumikia yeye hapa duniani.
Tena hayo yote ni sehemu ndogo sana, au ni kipande kidogo sana katika utumishi wa mtu katika kazi ya Mungu. Hayo mengine yote yanakuja yenyewe kwenye utumishi wa mtu akiwa na bidii ya kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote, kwa nguvu zake zote, kwa akili zake zote, na kwa roho yake yote.
Mungu akubariki sana.
Samson Ernest.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana.