Isaya 49:8(a)
Bwana asema hivi, wakati uliokubalika nimekujibu.

Shalom watu wa MUNGU.

Kuna mambo mengi MUNGU anatenda kwetu na nimeona nisikalie kimya, basi japo nilete mawili.

Lengo ni kumwinua KRISTO na kumtia moyo wa imani mtu fulani.

Sasa situmii miwani tena.

Mwaka jana nilipoteza miwani yangu ya kusomea, nilisikitika sana na jambo la kwanza nilijiuliza nitafanyaje kuhusu kujisomea Neno la MUNGU.

Kama wiki hivi nikawa namwomba MUNGU nipate miwani nyingine lakini wapi.

Siku moja nikiwa huko vijijini kwenye shughuli zangu nikabeba tu Bible kwa imani nikaelekea mlimani penye  madhabahu ninapokutanaga na MUNGU kila siku.

Baada ya maombi nikafungua Biblia yangu kwa imani, niliishia kutokwa machozi ya furaha kwa kuwa niliweza kusoma vizuri Neno la MUNGU bila miwani.

Miezi imepita, kwa kweli nimemthibitisha  BWANA kwamba ameniponya; sasa ninaona. Sibebi tena vikopo vya miwani.

Wewe mwenye tatizo kama nililokuwa nalo pokea Neema ya uponyaji kwa jina la YESU; na si lazima miwani yako ipotee kwanza kama ilivyotokea kwangu. Mungu ana njia nyingi.

Simu inafanya kazi kimiujiza.

Simu hii ina changamoto nyingi tangu mwaka jana October, ikafika mahali nikamwambia Kiongozi wetu Samson akiona  kimya nipo na hilo tatizo, akaniambia; Mungu atakupa simu nyingine baba.

Sasa wakati natembea katika imani ya kupata simu nyingine, mara tena display ikafa ndiyo ikawa haifanyi kazi kabisaa.

Moyoni mwangu nikajiuliza tafakari ya Neno la MUNGU  nitatumaje Chapeo Ya Wokovu; mke wangu akaniambia niwe natumia ya kwake.

Nikajihoji tena, kwa sasa nipo mjini sawa, je  nitakaporudi vijijini kwenye shughuli zangu itakuwaje!

Siku moja nikiwa tuu naishikashika hii simu, nikagundua kuna namna nikiibonyeza na kushikilia mahali  hapohapo, naweza kuandika ujumbe kama ninavyofanya sasa. Japo mara kadhaa unafutika wote hivyo inabidi kuanza tena!

Mungu kanisaidia niendelee kuwa connected na CYW.

Kwa kweli mambo haya mawili kwangu yaliyotendeka mwaka jana mwishonimwishoni yamenipa darasa kujua jinsi MUNGU anavyojishughulisha na kila kinachotuhusu sisi watoto wake kwa wakati.

Nilikuwa siwezi kusoma bila miwani sasa nasoma; simu ikifa display ni tatizo ila si hii ninayotumia.

Utukufu wa 2020 utakuwa mkubwa zaidi.

MUNGU akubariki sana.
Shealtiely Molla.
+255738858888