Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai, tunapoendelea kusoma Neno la Mungu, kuna mengi yanazidi kujitokeza kwa wanaochukulia hili jambo kwa uzito.
Leo baada ya kuandika ukurasa 191 wa SOMA NENO UKUE KIROHO bonyeza hapa kusoma zaidi. Kuna dada yetu (….) ameshuhudia haya kwa uzito sana. Karibu sana;
Mwanzo niliamini Mungu wetu ni mmoja!! Nilipotakiwa kuokoka nilikubali kwa moyo mmoja kabisa kumpokea YESU KRISTO lakini niliendelea kuswali!!
1. Niliona vyote sawa!! Kusali na kuswali maana Mungu ni mmoja!!!
2. Nilikuwa na hofu ya kumkiri Kristo!! Nilihofu mazingira/watu watu walionizunguka, nikashindwa kumhofu Mungu aliyeniambia nibadili dini na kuokoka!!!
Kwa kuona Mungu ni mmoja niliendelea kushiriki mambo yote ya dini ya zamani!! Katika sikukuu na katika kufunga!! Nilikuwa nafunga na kujihesabia kwamba nimefunga kikristo lakini nafunga nao na kufuturu nao lakini maombi nafanya kama mkristo!! Sitokueleza ilikuwaje lakini nataka utambue jambo hilo ni baya zaidi ya unavyofikiria.
Mimi nilikuwa ndio kwanza nimempokea Yesu, ndio kwanza nimepata wokovu, sijui lolote lile kuhusu maisha ya wokovu maana nimeokokea huku (Oman) hakuna kanisa karibu yangu kusema nipate mafundisho, nilitegemea mitandaoni tu. Lakini Pamoja na uchanga wangu Mungu hakuniacha niendelee kufanya huo upuuzi niliokuwa naufanya, na nilipokataa kutii maonyo yake ilinigharimu. Tena ilinigharimu sana wala siwezi kusahau kabisa katika maisha yangu yote ACHENI MUNGU AITWE MUNGU, MATENDO YAKE NI MAKUU NA YA KUTISHA SANA.
KWANINI NIMEONGELEA HILI? MUNGU ALINIAMBIA KITU KIMOJA AMBACHO NIMEKISHIKA SANA, NISOME BIBLIA NA KUFANYA KILE AMBACHO NENO LAKE KUTOKA HUMO LINANIAGIZA KUFANYA. ZINGATIA, _ALISEMA NISOME BIBLIA TU, NA KUFANYA KILE KILICHOMO HUMO TU NA SI KWINGINEKO KOKOTE.
Nakueleza haya wewe ambaye ijapokuwa umemkiri Kristo lakini bado upo chini ya ibada za zamani ulizokuwa unaabudu kabla, ambazo zina sheria/utaratibu ambao upo kinyume na maandiko yaliyopo katika Biblia.
NAKUSISITIZA, CHUNGUZA KILA UNACHOKIFANYA KATIKA MAISHA YAKO YA KIROHO IWAPO KIPO KATIKA MAANDIKO, (BIBLIA TU.) MPENDWA NAKUSHUHUDIA LEO KWAMBA IWAPO HAKIPO KATIKA MAANDIKO, UNAPOTEA!! NA WALA HUNA YESU NDANI YAKO.
YESU ANAITAJI TULIFUATE NENO LAKE PEKE YAKE, NA KULITII, NA NENO LA KRISTO LINAPATIKANA KATIKA BIBLIA BASI. SASA KAMA UNAPOABUDU KUNA KITENDO MNACHOFANYA AMBACHO HAKIPO KATIKA BIBLIA AU KINAKWENDA KINYUME NA MAANDIKO, WAULIZE WAMEKITOA WAPIIII? AU WAULIZE KWANINI WANAFANYA UBATILI? WAAMBIE WAKUONYESHE MAANDIKO LA SIVYO HAMAAA!!! MTU ASIANZE KUKUAMBIA “unajua bhana…… unajua bhana…..!” KATIKA KUMWABUDU MUNGU HAKUNA unajua bhana…. KATIKA KUMWABUDU MUNGU KUNA KWELI, NA INATAKIWA UITAFUTE IYO KWELI ILI UISHI KATIKA KWELI HIYO. NA KWELI YOTE INAPATIKANA KATIKA BIBLIA, HAKUNA NENO MUNGU ALISAHAU KULISEMA/KULIFANYA KUPITIA WATUMISHI WAKE KWAAJILI YETU, KILA KITENDO KILIANDIKWA, NA KILA NENO LILIANDIKWA, ILI SISI TUPATE KUISHI KATIKA HILO. MTU YEYOTE ASIKWAMBIE ETI……. hili lilifanywa baada ya Biblia kutoka hivyo halipo katika Biblia!!!….. _HUO NI UONGO MKUBWAAA ZAIDI YA SANA. MUNGU HAWEZI KUMTOKEA MTU NA KUMPATIA MAONO YALIYOTOFAUTI NA MAANDIKO NA KUMWAGIZA AWAAMBIE WATU WAYAFUATE HAYO.
KATAA SHUHUDA NA MAFUNDISHO YANAYOKUTAKA UFANYE JAMBO LILILO KINYUME NA NENO LA MUNGU.
NARUDIA TENA; NASEMA HIVI, KAMA KUNA KITENDO CHOCHOTE MNACHOFANYA UKO KATIKA KANISA/JAMII YENU KISILOKUWEPO KATIKA MAANDIKO (BIBLIA) KIKATAEEEE.
SOMA SANA NENO LA MUNGU ILI UJUE KIKUPASACHO KUTENDA.
TENA NAKUASA KATIKA BWANA, USIJE UKAKATAA KUMKIRI KRISTO POPOTE PALE NA KWA YEYOTE, KWA KUMHOFU MWANADAMU. USIJE UKAFANYA JAMBO LOLOTE LILILO KINYUME NA MAANDIKO KWA KUMHOFU MWANADAMU/ KWA KUMUHESHIMU MWANADAMU/ KWA KUMFURAHISHA MWANADAMU/ KWA KUTAFUTA SIFA/ KWA KUTAFUTA MWENZA/KWA KUILINDA NDOA AU UDUGU AU KUILINDA KAZI.
TENA USIJE UKAIGIZA MAISHA FULANI KWA WATU, KUWA WEWE SI MKRISTO WAKATI NI MKRISTO (kama mimi nimekwambia nilikuwa nafunga ramadhani na wenyeji wangu wanajua nimefunga kama wao kumbe nimefunga kikristo na nasali kikristo) NA KUJIFARIJI ETI MUNGU ANACHUKULIA POA, NAKUAMBIA KAMA UKO HIVYO UJUE UNAYO MAPUNGUFU MAKUBWA NA YAKUPASA UTUBU HARAKA.
Wengi tunajidanganya na maneno haya;
1. Mungu anajua nilipo na mazingira niliyopo atanisamehe kwa sasa maana nikiwa katika mazingira mazuri nitafanya kama anavyotaka.
2. Haiwezi kuwa ni tatizo maana Mungu anatazama moyo wa mtu na ananiona moyoni kwamba nimemkiri haya ya kimwili hayana maana.
MPENDWA WANGU KATIKA BWANA, TAMBUA MUNGU ANATAZAMA UNAVYOMKIRI NDANI YA MOYO NA NJE KATIKA MAZINGIRA UNAYOISHI, YAWEZEKANA KABISA MUNGU AKAWA AMEKUWEKA SEHEMU FULANI ILI AKUTUMIE HAPO. ILI UFANYE KITU HAPO NA KIJULIKANE KUWA KIMEFANYWA NAYE(YESU), SASA JIULIZE, IWAPO WEWE UMEMKIRI YESU MOYONI NA SI KATIKA MWILI NA ROHO, UNAFIKIRI YEYE ANAFANYA VIPI KAZI NDANI YAKO? USIOGOPE KITU WALA MTU YEYOTE, UMEAMUA KUMPOKEA YESU JIONYESHE KUWA WEWE NI WA YESU, NA YESU YU NDANI YAKO.
YESU ANATAKA AKIFANYA KAZI KUPITIA WEWE IJULIKANE KUWA NI YEYE ALIYEIFANYA, ILI HAO WALIOKUZUNGUKA, AMBAO PENGINE BADO HAWAJAMPOKEA YESU/HAWAMWAMINI/HAWAMJUI KABISA WAIONE KAZI YAKE NA WAMPE UTUKUFU, WASEME YESU NI MUNGU, WABADILI NIA ZAO,WAMUAMINI NA KUMFUATA. Danieli 3:1-30, 6:3-27.
Kama huwezi kumkiri Mungu (Yesu) katika mazingira yoyote, ni ngumu sana kumuona akitenda jambo maishani mwako. Kila jambo lina kusudi la Mungu, wakati mwingine anaweza kuwa amekuweka katika mazingira hatarishi ili akuinue. Acha kumkana na kufanya uovu, kuwa na msimamo kama Yusufu MWANZO 39:7-9.
Kuna wakati tunakuwa katika mazingira ya ajabu sana, au tunaishi na watu wa ajabu sana na kama haupo makini, utamkufuru Mungu sana bila kujijua.
Mimi nilikuwa napenda kusikiliza nyimbo za injili katika simu wenyeji wangu wakanizuia, nikaacha.
Nikaona isiwe tabu, nikawa naimba (si nina kinywa bwana?) kwanini nisimsifu Mungu kwa hicho? Napo nukazuiwa!! Nikaacha!
Nikaona isiwe tabu nina roho, nikaanza kuimba rohoni na kumsifu Mungu saaaanaaaa tu. Tena na vigeregere napiga uko rohoni, (Chezea Yesu wewe) majuzi kati niliitwa, nikawekwa kitako kabisa na bosi wangu, akaniambia hata kuimba rohoni humu ndani hataki. Yaani nikiwa karibu naye, garini au popote nisiimbe kabisa hata kwa roho, na akasema nyumba yake haitaki hizi nyimbo zangu. Nikakubali!! Maana jinsi alivyo mtu mzima tena na wazifa alionao, na jinsi alivyoongea nami kwa kusihi na kuomba, nilijikuta nakubali tu na akasema ASANTE KWA KUNIELEWA.
Lakini wanasema mzoea wima kukaa hawezi, Nishazoea kuimba! Haikupita muda nikaanza kuimba tena. Hata sikujijua sasa jana akanifuata, akabwata, hapa hakubembeleza bali alitumia amri.
Nikamuuliza kwani wewe ni shetani? Au shetani una undugu naye? Au una mapepo? Mimi naimba nyimbo za kumsifu BWANA wewe unanizuia kwanini? Akajibu mungu hazipendi!! Nikamuuliza Mungu yupi uyo asiyetaka kusifiwa? Akanijibu zinamuumiza kichwa sana akizisikia, nikamuuliza unazisikiaje na wakati naimba rohoni?
Nikamwambia sasa sikia, kwa hapa kumradhi, utake au usitake LAZIMA NIIMBE. nyie mnashinda mnapiga miziki katika tv, radio, simu na kutikisa mabega mnatikisa kabisa kichwa hakiumi. Lakini mimi naimba kwa sauti ndogo kabisaaa ya rohoni alafu kichwa kinawauma? Mtu asiniambie tena eti nisiimbe! Mkiona kero nifukuze kazi lakini lazima nimsifu Mungu wangu.
Nimewaambia mtu akaniambia tena habari za kuimba, badala ya kuacha nitaimba kwa sauti!! Na kama naimba rohoni vichwa vinawauma, mjue nikiimba kwa sauti vitapasuka kabisa.
Huu ni ushuhuda wangu kwa ufupi, nilikuwa nakupatia ushuhuda wa kweli wa mazingira tunayoishi yanavyoweza kukubana sana usimwabudu Mungu. Shetani ana njia nyingi za kutumia, usipokuwa makini utakuwa mtumwa wake!
MATHAYO 10:32-33, 7:24, 4:4, MARKO 8:34, LUKA 14:27, 6:46-49. Ipitie hiyo mistari na Mungu atakubariki sana.
Ujumbe wangu kwako, kuwa radhi kwa lolote kwa ajili ya Bwana.
Mungu akubariki sana.