“Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa”, Mk 7:27 SUV.

Kwanza kabisa unapaswa kuelewa kuwa Yesu aliposema “watoto” alimaanisha Waisraeli.

Yesu alionesha wazi kuwa injili ilitakiwa ipelekwe kwanza kwa Wahayudi.

Leo Yesu anatutaka tupeleke kwanza injili kwa wale wasioamini, wale ambao hawajapata neema ya wokovu.

Bila kujalisha kabila, tunapaswa kuwahubiria watu wote habari njema za Yesu.

Kufanya hivyo utakuwa umefanya jambo la msingi sana katika maisha yako ya wokovu.

Hatupaswi kubaki kuwalaumu watu wanaoabudu miungu mingine, tunapaswa kuwahurumia na kuwaeleza habari njema za Yesu Kristo.

Hili ndilo agizo kuu kwetu wafuasi wote wa Yesu Kristo, ukimfanya mwingine kuwa mfuasi wa Kristo utakuwa umefanya jambo la msingi sana katika maisha yako.

Soma neno ukue kiroho
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081